Hatimae gwiji wa Man Utd, Ryan Giggs ameamua kuondoka klabuni hapo baada ya kuitumikia kwa miaka 29 akiwa mchezaji na kocha msaidizi.

Giggs anaondoka baada ya kukataa ofa ya msaidizi wa meneja mpya wa klabu hiyo Jose Mourinho.

Kabla ya kufanya maamuzi hayo, Giggis ambaye alikuwa anacheza nafasi ya kiungo wa pembeni wakati wa utawala wa Sir Alex Ferguson, aliwahi kufanya kazi kama msaidizi wa David Moyes na Louis van Gaal ambaye alifanikiwa kubeba Kombe la FA.

Giggs mwenye umri wa miaka 44, alijiunga Man United mwaka 1987 akiwa anasherekea siku yake ya kuzaliwa wakati akitimiza miaka 14.

Alitokea timu ya watoto ya Manchester City.

18 Wafariki kwa Kulipukiwa na Bomu Somalia
Givanildo Vieira de Sousa Atimkia China