Jeshi la Polisi mkoani Arusha, linawashikilia watu wawili Loshiri Lawai (35), mkazi wa Olkokola na James Samwel (45), mkazi wa Tengeru wakiwa na meno mawili ya tembo .

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Justine Masejo amesema watu hao walikamatwa huko katika Kijiji cha Shambasha Wilayani Arumeru wakiwa na meno hayo ambayo walikuwa wameyapakia katika pikipiki Na. MC 509 BVG aina ya Kinglion.

Amesema, jeshi hilo kwa kushirikiana na Askari wa usimamizi wa Wanyapori wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano wakiwa na nyama ya twiga na Pundamilia zikiwa na ngozi pamoja na vichwa viwili vya Pundamilia.

Amewataja waliokamatwa kuwa ni Richard Piniel (23), Japhet Philipo (30), Lameck Ezekiel (23) wakazi wa Ngusero,  Peter Piniel (27) na Laila Issa (43) wakazi wa Morombo Jijini Arusha ambapo walikuwa na pikipiki zenye namba za usajili MC 141 CWL aina ya Sinoray, MC 983 CRG aina ya KingLion, MC 324 BXT aina ya Kinglion na bajaji aina ya Maxima namba MC 574 DBW.

Aidha uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo umebaini kuwa watuhumiwa hao wamekua wakijihusisha na biashara hiyo haramu, na wanaendelea kuhojiwa na pindi upelelezi utakapokamilika majalada yatapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Polisi Moro yamuita dereva tukio la kupigwa na Askari
Arsenal yamuweka kiporo Mikel Arteta