Utafiti uliofanywa na Chuo kikuu cha Havard nchini Marekani uliowashirikisha wanawake 2000 na kubainisha kuwa uwezo wa mwanamke kushika ujauzito hupungua kadri umri unavyosonga na imeonekana kuwa mwanamke anaweza kuongeza uwezo wa kupata ujauzito kama mwenza wake atakuwa na umri mdogo.
Umri wa mwanamke unaweza kuwa tatizo lakini. dawa ni kuwa na mwanaume aliyemzidi umri kwani anakwenda kuyaamsha” amesema Daktari Gillian Lockwood.
Watafiti walisema kuwa wanawake wana bahati sana kwani mbegu za uzazi wa mwanaume waliowazidi umri huyapa nguvu mpya mayai yao.
Na utafiti huu ulibainisha kuwa wanaweke wenye wenza waliowazidi umri au kuwa sawa nao hawakufanikiwa kushika ujauzito kwa haraka tofauti na wanawake wenye waunaume wenye umri mdogo maarufu kama Ben ten.
Wanawake wenye umri kati ya miaka 35 au 40 wenye wenza wa umri wa chini ya miaka 30 walifanikiwa kushika ujauzito haraka.
Lakini pia utafiti huu ulibainisha kuwa wanawake chini ya umri wa miaka 30 wenye wenza wa kuanzia miaka 40 kwenda juu hawakushika ujauzito kwa urahisi ukilinganisha na wale wenye wenza wa umri wa kati ya miaka 30 hadi 35.
Mwandishi wa kitabu cha The Male Biological Clock, Harry Fisch amesema kuwa sababu kubwa ya wanaume wenye umri mdogo kuwa na uwezo wa kumpa mwanamke mwenye umri mkubwa ujauzito ni mwanaume mwenye umri mdogo huwa na mbegu nyingi na zinazokwenda kwa kasi ukilinganisha na yule mwenye umri mkubwa.
Harry ameongezea kuwa kadri umri unavyozidi kwenda kwa mwanaume wingi wa mbegu na kasi yake hupungua.
Hivyo wataalamu wa afya ya uzazi wanashauri wanawake kuzaa kabla ya umri huo ili kuepuka madhara anayoweza kuyapata iwapo atachelewa kujifungua, na watafiti wanasema iwapo mwanamke atachelewa kuzaa ana hatari kubwa ya kujifungua mtoto mwenye kasoro za kimaumbile au kuwa njiti kabisa.