Imeelezwa kuwa wakati wa ujauzito, mwili huzalisha damu na maji kwa wastani unaokadiriwa kufikia hadi asilimia 50, ili kukidhi haja ya mtoto anayekua kwa kasi tumboni na kupelekea kuvimba kwa baadhi ya viungo vya mwili wa mama mjamzito.
Uvimbe huo wa kawaida (adema) mara nyingi huonekana kwenye mikono, miguu,nyayo na usoni.
Jambo ambalo wengi wamekuwa hawafahamu ni kwamba, kuongezeka kwa maji wakati wa ujauzito husaidia kuulainisha mwili ili uweze kutanuka na kuhimili ukuaji wa mtoto aliyepo tumboni.
Kwakuwa umbo la mtoto huongezeka siku hadi siku, nilazima mwili wa mama utanuke pia kukabiliana na hali hii, na kuziandaa nyonga ili ziweze kuwa na uwezo wa kupanuka ipasavyo wakati wa kuzaliwa mtoto.
Ili kukabiliana na tatizo hili mama amjamzito anatakiwa kufanya mazoezi mepesi tu kila siku hasa yanayohusisha kutembea.
Kufanya kazi kidogo za nyumbani ambazo zinaruhusu kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine, haishauriwi kulala sana kila muda, mazoezi nimuhimu sana.
Somo hili limeandikwa kwa msaada wa ukurasa unaotoa elimu ya afya ya binadamu, Afyainfo.