Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amehamia rasmi Jijini Dodoma na kwenda kujiandikisha kwenye daftari la orodha ya wapigakura katika kituo cha Sokoine kitongoji cha Sokoine wilayani Chamwino.

Akizungumza na wananchi waliokuwepo kwenye kituo cha kujiandikishia, Rais Magufuli amesema ameshahamia rasmi makao makuu ya nchi na kuwaahidi wananchi wa Chamwino kuwa tatizo la maji walilonalo litafanyiwa kazi haraka.

” Nimehamia rasmi Dodoma, nimejiandikisha katika eneo langu na nitapiga kura hapa hapa tarehe 24 kuwachagua viongozi wangu wa mtaa” amesema Rais Magufuli.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2016 Serikali ya awamu ya tano ilihamia rasmi jijini Dodoma na Aprili 2019 Rais Magufuli alizindua mji mpya wa Serikali, ambao ndiyo makao makuu ya wizara zote.

Eliud Kapchoge aliachiwa na wenzake kuvunja rekodi
Makala: Muasisi wa Tuzo za Nobel, ‘mfanyabiashara wa vifo’ alivyourudia ubinadamu