Wanawake wazee kutoka umoja wa wanawake UWT kata tatu za Ramadhani,mji mwema na Njombe mjini zilizopo halmashauri ya mji wa Njombe, wameendelea kusisitiza uwepo wa asilimia 50 kwa 50 katika nafasi mbali mbali za uongozi nchini.

Wameyasema hayo mkoani Njombe katika maadhimisho ya wiki ya wanawake na kumbukumbu ya kumuenzi Rais wa awamu ya kwanza wa jamhuri ya muungano wa Tanzania yaliyofanyika  katika ukumbi wa Turbo mjini Njombe.

Miongoni mwa wanawake walioshiriki maadhimisho hayo ni pamoja na Etinale Kiwale, ambao wanaomba serikali kuendelea kusimamia usawa katika nyadhifa mbali mbali za uongozi kwa kuwa wanawake pia wamekuwa wakifanya vizuri katika nafasi wanazopewa.

“Ninawapongeza sana wakina mama wanaoendelea kuongoza vizuri,lakini na ninyi mliopo madarakani endeleeni kuzungumza kwa ufasaha huku mkiwa viongozi bora, na sisi tunaendelea kusisitiza 50 kwa 50 tuendelee kuwa kwenye uongozi”alisema Rahabu mwandawa.

Angela Mwangeni ni mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe amesema katika kumuenzi mwalimu Nyerere ni lazima wanawake waweze kujitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa ili kudumisha demokrasia nchini.

Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Merry Lwiva amesema umoja wa wanawake ndio wanaotoa ushindi katika uchaguzi, hivyo amewataka watanzania kuendelea kuenzi fikra za mwalimu Nyerere, kazi zake pamoja na matendo yake.

“Wanawake pia tunakumbuka na kumuenzi mwalimu Nyerere,lakini pia katika kumbukumbu hizi tuendelee kuenzi fikra zake, kazi zake na hata matendo yake,kwa kuwa juhudi zake zimetuletea misingi bora ya utawala katika nchi yetu” alisema Merry

Aidha amewaagiza viongozi wanaotokana na chama cha mapinduzi kuhakikisha wanawasaidia wananchi kutatua matatizo pindi wanapofika katika ofisi zao.

Jafo ataja Mikoa iliyozorota uandikishaji, wakuu wa mikoa kitanzini
Serikali yasaini mkataba kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi