Baada ya klabu ya Aston Villa kushindwa kufuzu kucheza michuano ya ligi kuu ya Uingereza msimu ujao John Terry ametangaza kuondoka katika klabu hiyo.

Terry ambaye alijiunga na klabu hiyo mwaka 2017 anaondoka klabuni hapo baada ya kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja, ambapo ndani ya mkataba huo kulikuwa na kipengele cha kuongeza mkataba kama Aston Villa ingepanda daraja na kuingia Ligi Kuu.

Nahodha huyo wa zamani wa Uingereza amesema meneja wa Villa Steve Bruce amekua mtu muhimu kwake na amejifunza mengi ambayo hatayasahau maishani lakini ameumia sana baada ya Aston Villa kushindwa kufuzu kucheza ligi kuu msimu ujao.

Terry ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 37, alikuwa akipokea mshahara wa paundi 80,000 kwa wiki katika klabu ya Aston Villa. Hata hivyo Terry bado hajasikika akisema ataenda wapi baada ya Villa.

 

Manchester City waweka kambi mjini Naples, Italia
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 31, 2018