Kufuatia kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu kama Scorpion, Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemuhukumu miaka 7 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumjeruhi na kumsababishia upofu Said Mrisho.

Mnamo Septemba 6, 2016 saa 4 usiku maeneo ya Buguruni Dar es salaam, Scorpion alifanya tukio la unyang’anyi ambapo aliiba cheni ya Silva yenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000, simu ya mkononi na fedha taslimu Shilingi 330,000 vyote vikiwa na thamani ya Sh 474,000 mali ya Said Mrisho.

Inadaiwa kuwa kabla na baada ya kufanya tukio hilo, Scorpion  alimchoma visu Mrisho sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo machoni, tumboni na mabegani ili kurahisisha kupata mali hizo.

kufuatia tukio hilo  Said Mrisho ambaye mpaka sasa hana uwezo wa kuona baada ya kutobolewa macho yake yote mawili ameamriwa na mahakama kulipwa faini ya milioni 30  kama namna ya fidia.

Pia Mahakama hiyo imemuachia huru Scorpion katika kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Frola Haule.

Hakimu Haule amesema katika hukumu hiyo Mahakama ilijikita sehemu kuu tatu ikiwemo kama mlalamikaji, Said Mrisho  amepata majeraha ya hatari pamoja na kama Scorpion alitumia unyang’anyi wa kutumia silaha.

“Faini ilipwe wakati unatumikia kifungo, pia ni ruksa kukata rufaa kwa upande wowote kama haujaridhika,” – Hakimu Haule.

 

Hata hivyo Said Mrisho ameonekana kutoridhishwa na hukumu hiyo ya miaka ya 7 na kusema ni ndogo hivyo atapeleka ombi lake kwa Rais Magufuli.

Mpina akitwanga faini kiwanda cha Sanflag
Hukumu ya Sugu kujulikana leo