Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amekitoza faini ya Shilingi milioni mia moja Kiwanda cha Sunflag Tanzania Limited cha Jijini Arusha baada ya kukutwa na makosa mawili ambayo ni kuzalisha na kuuza nyavu bila kuwa na leseni kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Amesema mkakati uliopo kwa sasa ni kuwabaini watengenezaji na wasambazaji wote wa zana haribifu za uvuvi ikiwa ni pamoja na vyavu zisizoruhusiwa kisheria.
“Operesheni ya kuwabaini na kuwachukulia hatua wafanya biashara wakuu wanaofadhili na kuendeleza  biashara ya uvuvi haramu ni ya kudumu ambapo mkakati uliopo  sasa ni kuwanyang’anya na kuwafutia lesseni zao za biashara” alisisitiza Mpina
Aidha, amewaonaya wafanyabiashara wanaosafirisha samaki na mazao yake katika nchi jirani za Uganda, Rwanda, na Burundi waache mara moja.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ajay Shah amekiri kutenda makosa hayo na kueleza kuwa kiwanda kimekuwa kikiendelea kutengeneza nyavu hizo bila kujua kuwa kilikuwa hakizingatii sheria za Uvuvi.

Majaliwa: Hakikisheni mnatokomeza uvuvi haramu
Said Mrisho aikatia rufaa hukumu ya Scorpion