Mwenyekiti wa kamati ya sheria na hadhi za Wachezaji wa (TFF) Said Soud, amewataka Wachezaji wa Soka la Bongo kuwa Makini wanaposaini Mikataba na Klabu zinzowasajili.
Soud ametoa rai hiyo kwa wachezaji, kufuatia sakata la Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ la kujaribu kuvunja Mkat5aba wake na Waajiri wake Young Africans mwishoni mwa mwaka 2022.
Kiongozi huyo amesema Wachezaji wa Soka la Bongo wnaapaswa kuwa makini wanaposaini Mikataba yao kabla ya kufikai maamuzi ya kuisaini, ili kujiepusha na matatizo ya kisheria kama yaliyomsibu ‘Fei Toto’.
Amesema Wachezaji wengi huwa wanasaini mkataba baada ya kusoma ukurasa unaoonesha mshahara watakaolipwa lakini hawapitii karatasi zenye vifungu vyenye masharti ya utekelezaji wa Mkataba husika.
“Feisal alisimamia kifungu kimoja wakati mkataba huundwa kwa vipengele vingi, unapaswa uvisome vyote kwa pamoja”
“Ninawashauri Wachezaji wetu wawe makini sana katika suala la Mikataba wanayoisaini, wanapaswa kujipa muda na kujua kilichoandikwa ndani, wasiangalie sehemu ya mshahara tu,” amesema Said Soud