Uongozi wa Geita Gold FC umetoa ufafanuzi wa kina kuhusu sakata la Mshambuliaji George Mpole ambaye anahushwa na taarifa za kutoroka Kambini kwa shinikizo la kulipwa sehemu ya fedha anayodai klabuni hapo.

Sakata hilo liliibuliwa jana Jumanne (Novemba 08) na Mwenyekiti wa klabu hiyo Constatine Morandi alipohojiwa na Kituo cha Radio cha EFM, ambapo alisema: “Mpole ni mchezaji wa Geita anahitajika kambini haraka na taarifa za madai sio za kweli hakuna anachotudai na hawezi kuwa mkubwa zaidi ya klabu anahitajika uwanjani aonyeshe ni mchezaji mzuri kwa kucheza sio kutumia alichokifanya msimu uliopita”

Hata hivyo Afisa Habari wa Klabu ya Geita Gold FC Samwel Didda leo Jumatano (Novemba 09) ametoa ufafanuzi akisema: “Geita Gold haijafikia level hiyo kwamba mchezaji anagoma kwa sababu maslahi.Tuna heshimu haki za wachezaji, hii ni tasisi iliyo chini ya Halmashauri kwa hiyo miongozo yake inakwenda sambamba na ya miongozo ya kiutumishi”

“Ni kwa vile taarifa zimekuwa zinatoka bila ya kuwa na uthibitisho lakini kwa sasa kilakitu kipo sawa na tunaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya KMC”

“Kwa wachezaji ambao tumekamilisha kwa kiwango kikubwa mahitaji yake nadhani ni George Mpole. Si tu kile alichokihitaji kabla hajasaini mkataba lakini hata baada ya kusaini mkataba, vyote vilikwenda sawa”

“George aliondoka baada ya mchezo wetu dhidi ya Coastal Union tuliocheza Tanga, aliondoka asubuhi wakati tunajiandaa kuondoka Tanga kurudi Geita kujiandaa na mchezo dhidi ya Namungo”

“Alitoa taarifa kwa meneja wa timu kwamba haturudi Geita kwa sababu anakwenda Dar es Salaam kujutana na daktari wake kwa sababu anahisi anamaumivu ya paja”

“Viongozi wakauliza ripoti yake kwa madaktari wa timu wakasema hawana taarifa zake. Viongozi wakataka kukutana na George kumuuliza kuhusu tatizo lake pengine madaktari wetu wangeweza kumsaidia tatizo lake lakini hakuja”

“Tukasafiri kwenda Dar kwa ajili ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, George alikuja mazoezini na Kocha Fred Felix Minziro akamruhusu kufanya mazoezi”

“Siku ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting hakuwa kwenye mpango wa mwalimu, baada ya mchezo huo tuliondoka kurudi kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga lakini George hakurudi akaendelea kubaki Dar”

“Kwa hiyo sisi tunaendelea kuamini kwamba hayupo sehemu yake ya kazi! Lakini tunaona kwenye mitandao anasema anaidai Geita Gold, aulizwe anadai nini?”

Hersi Said: Tupo tayari kukabili Club Africain
George Mpole: Sitamani kurudi Geita Gold FC