Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo BAWACHA Zanzibar, Sharifa Suleiman amewataka Wanachama 19 waliofukuzwa kuacha kutumia Nyaraka, nembo na bendera za chama hicho
Amesema, Wabunge hao si Viongozi wala Wanachama wa CHADEMA tangu Novemba 27 walipovuliwa nafasi zao na kufukuzwa uanachama kwa kushiriki katika uapisho.
”Wabunge hao wa Viti Maalum wanashirikiana na Mamlaka kuwahadaa baadhi ya Viongozi wa BAWACHA kwa fedha ili wafike Dar es Salaam kwenye mkusanyiko wanaouandaa kwa Jina la CHADEMA”
Katika taarirfa yake aliyoitoa Desemba 16, 2020 Makamu huyo ameueleza umma kuhusiana na kuandaliwa kwa kongamano la wanawake wa CHADEMA ambalo halina uhalali huku akidai taarifa za kongamano hilo wameshalithibitisha .
Aidha kwenye taarifa yake Sharifa amesema kongamano hilo linaandaliwa na watu wasio na malengo mema kwa chama chao ambao wanawarubuni baadhi ya viongozi na akinamama wa baraza kwa fedha ili kushiriki kongamano hilo.