Klabu ya Azam FC imetthibitisha kumsajili Mlinda Lanho Ahmed Ali Suleiman ‘Salula’ akitokea KMKM ya Zanzibar.
Azam FC imemsajili Salula kwa mkataba wa miaka miwili, huku wakiamini uwepo wake utaingeuza chachu katika ulinzi wa lango lao msimu wa 2021/22.
Mlinda Lango huyo mwenye umbo kubwa, amesaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’.
“Salula ni mmoja wa makipa hodari, akiwa ndio tegemeo katika timu ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’, anakuja kuongeza nguvu katika eneo la langoni kwenye timu yetu.” amesema Popat
Huo unakuwa usajili wa saba kwa Azam FC kuelekea msimu ujao, tukiwa na nia ya dhati ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CC).
Wachezaji wengine waliowasajiliwa klabuni hapo ni beki wa kushoto, Edward Manyama, kiungo mkabaji, Paul Katema (Zambia), viungo washambuliaji, Charles Zulu (Zambia), Kenneth Muguna (Kenya) na washambuliaji Rodgers Kola (Zambia), Idris Mbombo (DRC).