Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Taifa, Samia Suluhu Hassan amepata kura 1914 na kura moja ya hapana huku Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania bara, Abdulrahman Kinana akipata kura 1,913 na mbili za hapana na Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi akipata kura 1912 na kura tatu za hapana.
Matokeo ya kura hizo, yanafuatia uchaguzi uliofanywa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM uliofanyika Desemba 7, 2022 katika mkutano wake wa 10 wa CCM Taifa ambapo pia Wajumbe wa Wajumbe wa NEC walichaguliwa na kwa upande wa Tanzania Bara upande wa Wanaume ni Igaga Mahenda(845), Innocent Bashungwa(720), Stephen Wasira(680) na Joseph Musukuma (587).
Wengine ni Richard Kaselela (574), Wambura Mwita (545), Hussein Bashe (510), Nape Nnauye (508), Josephat Gwajima (497), Januari Makamba (452), Mwigulu Nchemba (450), Anamringi Macha (435) na Ibrahim Msengi (415).
Picha: Mwenyekiti wa CCM ashiriki zoezi la kupiga kura
Aidha kwa upande wa Wanawake Tanzania Bara walioshinda ni Christina Mndeme (761), Angelina Mabula (770), Ashatu Kijaji(764), Hellen Makungu(755), Fenela Mukangara (747) na Angellah Kairuki (730).
Kwa upande wa Wajumbe wa NEC Visiwani Zanzibar Wanaume ni Makame Mbarawa (798), Issa Haji Ussi (704), Joseph Abdalla Meza (701), Shaka Hamdu Shaka (698), Mohamed Said Mohamed (651), Hamza Khamis Chilo (637), Amin Salum Amour (610) na Mohamed Habib Mohamed (583).
Wengine ni Mbarouk Nassor Mbarouk (554), Abdulhafar Idrissa Juma (521), Nasir Ali Juma (419), Khamis Mbeto Khamis(416), Mbaraka Saidi Rashid(379), Abdullah Sadala Mabodi(363).
Upande wa Wanawake walioshinda ni Saada Mkuya (653), Tabia Mwita (666), Najma Murtaza Giga (686), Leila Ngozi (702), Amina Hamis Omary (579) na Mvita Mustapha Ali aliyepata kura 547.