Nyuso za wasichana 108 wa shule ya Chibok ,ambao walitoweka miaka nane baada ya kutekwa na waasi wa kundi la Boko Haram zimechongwa kwa udongo kwa ushirikiano kati ya msanii wa Ufaransa Prune Nourry, wanafunzi wa chuo kikuu, wafinyanzi wataalamu na familia za wahasiriwa.

Wasichana hao, ambao bado hawajapatikana walitekwa na kundi hilo lenye itikadi ya kiislam nchini Nigeria mwaka 2014 na wanakumbukwa katika maonyesho mapya ya vinyago jijini Lagos katika mtindo wa vichwa vya kale vya terracotta vya Kinigeria viitwavyo “Statues Also Breathe.”

Utekaji nyara wa watu wengi, awali ulizua ghadhabu duniani kote, na kufanya kauli mbiu ya “BringBackOurGirls” kuvuma kwenye mitandao ya kijamii na kutumiwa na watu mashuhuri akiwemo mke wa rais wa zamani wa Marekani, Michelle Obama.

Aidha, tangu kuanza kwa kampeni hiyo wasichana wapatao 160 waliachiliwa huru na makundi ya watekaji baada ya kuwa kizuizini kwa miaka mingi, na Habari za mateka sasa zimegeuka sehemu ya kujipatia fedha kwa watu kutekwa na kulipia uhuru wao.

Wabunge wa upinzani jela miezi sita kwa shambulio
Idadi ya vifo ajali Lori la mafuta yafikia 34