Imefahamika kuwa Mshambuliaji kutoka nchini Chile Alexis Sanchez alimpigia simu Meneja wa Klabu ya Arsenal, Mikel Arteta kwa ajili ya kumuomba arudi Emirates kwa mujibu wa ripoti.
Sanchez mwenye umri wa miaka34, atakuwa mchezaji huru mkataba wake utakapomalizika mwezi huu baada ya kuondoka Marseille, lakini tayari ameanza kupokea ofa nyingi.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United, alifunga mabao 18 wakati anakipiga Inter Milan msimu uliopita, na kwa mujibu wa ripoti Sanchez anataka kurejea Ligi Kuu England.
Arsenal imepewa muda wa kufikiria kama itakuwa tayari kumrudisha Mshambuliaji huyo ambaye amewahi kukiri kuipenda klabu hyo ya kaskazini mwa jijini London.
Sanchez alifunga mabao 80 ndani ya miaka mitatu aliyokipiga Arsenal, kabla ya kutimkia Man United mwaka 2017 hata hivyo hakung’ara sana.
Lakini Arsenal ipo bize kusaka wa chezaji hatari kwenye usajili huu wa kiangazi, na tayari inakaribia kuinasa saini ya Kai Harvetz kutoka Chelsea.
Habari kutoka Chile zimeripoti Sanchez anapambana kushawishi Arteta lakini ombi lake limekataliwa licha ya kumueleza nia yake ya kutaka kurudi Arsenal.
Imeelezwa Sanchez anataka awe sehemu ya kikosi cha Arsenal ambacho kilikua hatari msimu uliopita, hata hivyo kikakosa ubingwa mbele ya Man City.