Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga amewahimiza wanachama wa Ardhi SACCO Ltd kuongeza ubunifu zaidi ili kuleta hamasa ya maendeleo na kuwavutia wanachama wengi zaidi kujiunga na Chama hivyo.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Mhandisi Sanga hii leo Desemba 14, 2023 jijini Dodoma, wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa Ardhi SACCOS Ltd Mkurugenzi wa Idara ya Miliki Wizara hiyo Dkt. Upendo Matotola amewataka wanachama hao kufanyakazi kwa bidii ili kufikia malengo ya SACCOS hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Milki Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Upendo Matotola akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga wakati wa kufungua mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Kuweka na Kukopa (SACCOS) cha Wizara ya Ardhi uliofanyika jijini Dodoma tarehe 14 Desemba 2023.

“Mkiweza kujiunga wote na Chama hiki, niwahakikishie mtapiga hatua kubwa sana katika kukabiliana na makali ya maisha pamoja na kujikwamua kiuchumi kama watumishi,” amesema Dkt. Matotola.

Mkurugenzi wa Idara ya Milki Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Upendo Matotola akiwa katika picha ya pamoja na baaadhi ya wanachama wa Chama cha Kuweka na Kukopa (SACCOS) cha Wizara ya Ardhi wakati wa mkutano Mkuu wa mwaka wa chama hicho tarehe 14 Desemba 2023.

Chama hicho kina wanachama 354 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo kulikuwa na wanachama 295 tangu SACCOS hiyo ianzishwe mwaka 2021,huku Wizara hiyo ikikadiriwa kuwa na watumishi takriban 2,300.

Aidha, Dkt. Matotola ameongeza kuwa kila mwanachama anawajibu wa kuwa balozi na kuhamasisha watumishi wengine wa Wizara hiyo kujiunga na Chama hicho, huku Gidfrey Machabe kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akisema malengo ya Ardhi SACCOS Ltd ni kuwawezesha watumishi wa Wizara hiyo kujikwamua kiuchumi.

Msiwazalishie Wananchi migogoro - CHADEMA
Benchikha kusajili mshambuliaji Simba SC