Wakati dunia bado ipo kwenye majonzi juu ya matendo maovu ya soka, kalamu ya Katrin Bennhols wa New York Times (Jarida kubwa duniani) alifichua juu ya manyanyaso ya Kingono baada taarifa ya Andrew .Woodward
Ni huyu Senzo alitumia kalamu yake kuandika andiko “Football please save our future footballers” andiko lile pia lilitoa mbinu za kukabiliana na tatizo lingine lilotokea Nigeria, November 22,2016 aliandika Cyruacus Izuekwe juu ya Kocha Frank Darlington kulawiti wachezaji wadogo.
Aliikumbusha dunia kuhusu sheria za Academy ya soka, alikikumbusha chama cha soka Afrika Kusini juu ya umuhimu wa kuzingatia ile sheria, aliwakumbusha na walimsikia kwenye kuzingatia Kanuni za kutoa leseni za Academy, ni yeye pekee duniani alitoa majibu ya yale maswali.
Wakati wachezaji wengi wa Afrika wakistaafu wanaishi maisha duni sana, watu walitazama maisha ya wakina Phil Masinga aliefilisika 2011, David Mkandawire wa Martzburg United hana pa kulala sasa, Benedict Vilakazi anaishi kwa tabu, Afrika Kusini ilihitaji namna ya kuwasaidia
Senzo kwa utulivu mkubwa sana, katikati ya mateso ya wanasoka wa nchi yao akaja na majibu, aliachia andiko kubwa sana “Assisting Footballers with their retirement” la April 25,2018 lilikuja kuleta pumzi na mwelekeo mpya kwa wanasoka wao, anaheshimika sana na Mastaa kama Steven Pienaar na Benny McCarthy, wachezaji wanalisoma sana.
Kutokana na mambo yake, WFS ambao ni mkutano mkubwa wa sera za soka duniani walimuita atoe mawazo yake, ni kwenye kilele kama hiki PSG na Manchester City walipitisha mfumo wa Alama za vidole kwa ajili ya ulinzi wa viwanja, FIFA ikapika upya mfumo wa tiketi na soka la Italia kuchukua sura mpya.
Ni Senzo mwenye misimamo yake isioyumba aliwapa makombe Platnum Stars ila baada ya kupishana nao aliondoka zake 2017, msimu uliofata timu ilishuka daraja, ni yeye pia aliacha kazi Orlando Pirates kwa ajili ya changamoto mpya, ana uzoefu wa zaidi ya nyanja 50 kwenye utawala wa soka.