Kamati ya maadili ya shirikisho la soka duniani FIFA, ambayo ilikua na mkutano kwa muda wa juma moja huko nchini Usiwz, imeamuru rais wa shirikisho hilo kufungiwa kwa kipindi cha siku 90, ili kupisha uchunguzi wa ubadhilifu wa fedha unaokusudiwa kufanywa na serikali ya nchini humo.

Kamati hiyo ilikutana baada ya mwanasheria mkuu wa serikali ya nchini Usiwz, kufungua mashataka dhidi ya Blatter, aliyekaa madarakani tangu mwaka 1998, ambayo yanalenga kuchunguza malipo ya fedha yanayodaiwa kufanywa na kiongozi huyo kweneda kwa rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Paltini.

Mbali na tuhuma hizo za malipo ya paund million 13 yanayodaiwa kwenda kwa Platini, Blatter pia anatuhumiwa kwa kukubali kuidhinisha baadhi ya mikataba isiyokua na manufaa kwenye shirikisho la soka duniani FIFA.

Hata hivyo, wakati kamati ya maadili ya FIFA ikifikia hatua ya kumfungia Blatter kwa muda wa siku 90 ili kupisha uchunguzi, bado haijafahamika rais wa UEFA, Michel Platini atachukulia hatua ziki za kimaadili ndani ya shirikisho la soka barani Ulaya.

Platini ni mmoja wa waliotangaza nia ya kutaka kuwania kiti cha urais wa FIFA, ambacho kitampata mrithi wa Blatter katika uchaguzi uliopangwa kufanyika februali 26 mwaka 2016.

Mvua Yaharibu Mchezo Wa Kihistoria
Dk. Slaa Aanza Rasmi Kumpigia Kampeni Magufuli