Wadau wa michezo nchini wameendelea kumiminika kuichangia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys ili kuweza kutoa hamasa kwa wachezaji na viongozi.

Akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa amepokea Hundi ya shilingi Millioni 50 kutoka Kampuni ya SportPesa kwa ajili ya kuisaidia timu ya mpira wa miguu  ya vijana  chini ya miaka 17 “Serengeti Boys”.

Amesema kuwa Serikali itaendelea  kushirikiana na wadau wa michezo nchini katika kuhakikisha sekta hiyo inafanya vizuri zaidi kupitia mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi .

“Naishukuru kampuni ya SportPesa kwa kuiunga mkono Timu yetu  ya Mpira wa Miguu ya Serengeti Boys, hili ni jambo zuri na la kuigwa hivyo kama wizara ninaahidi  kuendelea  kushirikiana na wadau wote nchini ili kuweza kuinua michezo ” amesema Dkt. Mwakyembe.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka kampuni ya  SportPesa, Tarimba  Abbas  amesema  kuwa ametekeleza ahadi iliyotolewa na  kampuni yake katika kuhakikisha kuwa inaichangia timu ya Serengeti Boys.

Ziara ya Zuma Tanzania yaimarisha ushirikiano
Zahoro: sera ya utalii imepitwa na wakati, yahitaji mabadiliko