Beki wa zamani wa Real Madrid, Sergio Ramos amekiri kwamba aligoma kusaini mkataba mpya baada ya kupewa ofa na Paris Saint-Germain ili ajiunge na Sevilla.
Kauli hiyo aliisema baada ya beki huyo wa zamani wa Real Madrid kurejea Sevilla kwa mara ya kwanza tangu alivyoondoka katika jiji hilo miaka 18 iliyopita.
Akizungumza baada ya uhamisho kukamilika Ramos alisema: “Waliponipa nafasi ya kuchagua kwa sababu niliamini nimepata nafasi ya kuendeleza soka langu ambalo nilidhani limekwisha, sio kwa sababu ya pesa wala mkataba.
“Hisia zangu ndio zimenifanya nirudi nyumbani na sikutaka kusaini PSG, nataka kuisaidia timu kama kiongozi, naamini tutafanya mambo makubwa hapa.”
Wakati huo huo Ramos alibubujikwa na machozi baada ya kurejea katika timu yake ya utotoni wakati akitambulishwa.
Beki huyo akasema alijisikia vibaya alipozomewa na mashabiki alipocheza dhidi ya Sevilla wakati anakipiga Madrid. Na baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Sevilla mwaka 2018, mashabiki walimponda na kumdhilhaki.
Sevilla ilimsajili beki huyo akiwa mchezaji huru baada ya kuondoka PSG na kuna taaa Manchester United ilimnyemelea pia katika dirisha la usajili la kiangazi.
Ramos aliichezea Sevilla mechi 50 kabla ya kujiunga na Los Blancos mwaka 2005.