Serikali imeahidi kuboresha vituo vya Forodha Mkoani Kilimanjaro, kwa kuweka vifaa vya kisasa, kuboresha majengo ya ofisi hasa la mizigo, kuboresha mazingira ya Nyumba za Watumishi wa Kituo hicho na kuongeza vitendea kazi ikiwemo vile Mdaki (Scanner).

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande ameyasema hayo alipokuwa akifanya ukaguzi kwenye kituo cha forodha kilichopo katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro – KIA, wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili Mkoani Kilimanjaro.

Amesema, “ndani ya mwaka wa fedha 2023/24, Serikali itahakikisha inaweka kipaumbele kuwapatia Mdaki (Scanner) moja, Serikali itafanyia kazi changamoto nilizoziona na vituo vyote vya forodha nilivyotembelea tumeona hii changamoto na Serikali itahakikisha inalitatua.”

Aidha, Chande pia alitumia nafasi hiyo kuwaomba watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA, kufanya kazi kwa uadilifu ili kukuza ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha huduma wanazotoa kwa walipa kodi iwe ya wazi na kwa uzalendo.

TEHAMA: Kakere ataka maoni chanya maboresho Kidijitali
Barabara App kusaidia ujenzi miundombinu, kupunguza ajali