Katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 hadi Aprili 2023, Jeshi la Kujenga Taifa – JKT ilimepatiwa kiasi cha shilingi 7,000,000,000.00 sawa na asilimia 50.12 ya bajeti iliyoidhinishwa, Kiasi ambacho kimetumika kujenga na kukarabati miundombinu ya vikosi na makambi, pamoja na kuendeleza skimu ya umwagiliaji katika Kikosi cha Jeshi cha Chita.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa hii leo Mei 24 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Amesema, hadi kufikia Aprili 2023, Shirika la TATC limepokea kiasi cha fedha shilingi 12,000,000,000.00 sawa na asilimia 60.12 ya bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya kujenga uwezo na kuendeleza utafiti na kuhawilisha teknolojia ya magari.

Waziri Bashungwa ameongeza kuwa, Shirika la Mzinga liliidhinishiwa jumla ya shilingi 4,000,000,000.00. Hadi kufikia Aprili 2023, Shirika limepokea kiasi cha shilingi 3,805,911,630.00 sawa na asilimia 95.15 ya Bajeti iliyoidhinishwa na kuweza kutekeleza shughuli za maendeleo mbalimbali ikiwemo ukarabati wa majengo na miundombinu ya kiwanda.

Aidha, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuzipa kipaumbele shughuli za ulinzi kwa kutoa fedha kugharamia operesheni za kupambana na ugaidi, ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa Kikombo jijini Dodoma, kusafirisha wastaafu, madeni ya wazabuni, mafunzo na vifaa vya mifumo ya malipo na ununuzi wa magari ya makamanda na Wambata Jeshi.

Hatma ya Lionel Messi ipo mikononi mwake
Kabwe aondoka rasmi AS Vita, aitaja Simba SC