RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali yake inachukua hatua kubwa kufikisha mazao kwenye masoko, ili kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo nchini, huku Wakulima wa Tanzania wakipata bei nzuri ya mbaazi kutoka kuuza Shilingi 300 hadi kufikia Shilingi 2000.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Septemba 7, 2023 kwenye Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula linalofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Marais wa nchi 7 wa Afrika kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa chakula kwa nchi zao.

Aidha, Rais Samia pia amesema matumizi ya teknolojia katika kilimo cha umwagiliaji yanayotarajia kufanywa yatazidi kuiboresha sekta hiyo nchini na kuvutia watu wengi, wakiwemo vijana.

#RaisSamia #KeshoBora #AGRF2023.

Van Gaal: Argentina ilibebwa Kombe la Dunia
Serikali kuongeza uzalishaji Mbegu za Kisasa