Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kikosi cha Uholanzi Louis Van Gaal amedokeza matokeo ya Kombe la Dunia la FIFA mwaka jana nchini Qatar “yalitengenezwa” ili kumsaidia Lionel Messi kubeba kombe hilo akiwa na Argentina.

Messi aliiongoza Argentina kunyakua ubingwa wake wa kwanza na watatu wa Kombe la Dunia kwa nchi yake mnamo Desemba, mwaka jana, nyota huyo alipofunga mara mbili kwenye Fainali na kusaidia taifa hilo la Amerika Kusini kuishinda Ufaransa kwa Penati 4-2 kwenye Uwanja wa Lusail.

Awali Argentina walikuwa wameiondoa Uholanzi nje ya michuano hiyo katika hatua ya Robo Fainali baada ya kuwafunga kwa penati kufuatia sare ya mabao 2-2.

Van Gaal, ambaye alijiuzulu kama Kocha Mkuu wa Uholanzi baada ya kuondoka kwenye Fainali za Kombe la Dunia, alisema alifikiri mchezo wao dhidi ya Argentina ulikuwa wa kupangwa.

“Sitaki kusema mengi kuhusu hilo,” alisema Van Gaal alkiwaambia waandishi wa habari.

“Unapoona jinsi Argentina walivyofunga mabao yao na jinsi tulivyofunga mabao yetu, na jinsi baadhi ya wachezaji wa Argentina walivyovuka alama na hawakuadhibiwa, basi nadhani wote ulikuwa mchezo wa kupangwa.”

Alipoulizwa kufafanua alichomaanisha, Van Gaal alisema: “Namaanisha kila ninachosema.”

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 8, 2023
Mazao kufikishwa Sokoni, bei ya Mbaazi yapanda