Serikali imekamilisha miundombinu muhimu ikiwemo ya Maji, Umeme na Barabara kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi VETA mkoani Kagera.
Hayo yamesemwa mkoani humo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako mara baada ya kuzindua chanzo Cha Maji ambacho kitatumika kwa ajili ya kujenga Chuo hicho katika kijiji Cha Burugo, halmashauri ya Bukoba.
“Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwa nchi ya uchumi wa kati hadi ifikapo mwaka 2025 ili kutimiza malengo hayo ndiyo serikali imewekeza zaidi katika kujenga vyuo vya ufundi stadi ili kuwa na wataalamu wa kati na wa kutosha watakaotumika kwenye viwanda hapa nchini,”amesema Profesa Ndalichako
Aidha, Waziri Ndalichako pia ametembelea na kukagua ujenzi unaoendelea wa Chuo Cha Ufundi Stadi Karagwe ambapo amemtaka mkandarasi kuhakikisha kazi hiyo inakamilika katika muda uliopangwa.
Katika hatua nyingine, Ndalichako ameonyesha kutoridhishwa na hatua za ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi mkoani humo na kuzitaka mamlaka husika kutafuta ufumbuzi ili kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi.
Profesa Ndalichako pia alitembelea Shule ya Bukoba Sekondari ambayo paa za shule hiyo ziliezuliwa kufuatia mvua kubwa Iliyoambatana na upepo, hivyo kulazimika wanafunzi wa shule hiyo kuhamishiwa katika shule ya sekondari Ihungo na wengine katika shule ya Sekondari omumwani.
-
Aliyeikataa kesi ya Zitto kuhusu CAG asifiwa na CJ
-
Anusurika kifo kisa marejesho ya mkopo
-
Ushoga, usagaji shule za Tanga wamshtua Mahiza, akemea