Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandis Edwin Ngonyani amesema kuwa Serikali itajenga daraja la juu kwa ajili ya kivuko cha waenda kwa miguu (Over head Pedestrian Bridge) eneo la Kawe Bondeni jijini Dar es salaam.
Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa Niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
“Tatizo la kivuko cha waenda kwa miguu eneo la Kawe Bondeni hadi Jeshini Kata ya Mbezi Juu na Kawe Tayari limeshapatiwa ufumbuzi”,Amesema Kamwelwe.
Amesema kuwa kwa sasa Mkandarasi wa kujenga daraja hilo yupo kwenye hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi katika eneo hilo muhimu.
Hata hivyo ameongeza kuwa Serikali ina mpango wa kuweka taa za kuongozea magari katika Barabara ya Mwenge-Tegeta ambapo Mkandarasi ameshapatikana wa kuweka taa hizo katika makutano ya Afrikana na anatarajia kuanza kazi wakati wowote.