Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amefungua kongamano la Kisayansi la Hospitali ya Taifa Muhimbili na kusisitiza kuwa serikali imedhamiria kutoa muongozo mpya wa matumizi ya dawa ili kudhibiti matumizi holela ya dawa.
Amesema kuwa muongozo huo utasaidia kupunguza matumizi holela ya dawa ambayo yanachangia usugu wa dawa katika mwili wa binadamu.
“Muongozo huu mpya utakapotolewa utatumika katika Hospitali zote nchini na pia serikali tayari imeoredhesha dawa muhimu na dawa hizi zinapatika kwani serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka Shiling bilioni 30 hadi kufikia bilioni 269,” amesesisitiza Dkt. Ndugulile.
Aidha, Dkt. Ndugulile ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada zake za kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha inapunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
-
RC Morogoro apata ajali ndani ya Hifadhi ya Mikumi
-
LHRC yazungumzia utafiti wa misimamo mikali nchini
-
Waziri mkuu Majaliwa akamata Semi Trela 44 Bandarini
Hata hivyo, Muhimbili tayari imeanza kutoa huduma ya kupandikiza figo, kufanya upasuaji wa kuwawekea vifaa vya kuwasaidia watoto kusikia na sasa wataalam wengine wanajiandaa kwenda India ili kujengewa uwezo wa kufanya upasuaji wa kupandikiza Ini.