Serikali imesema kuwa inatarajia kupiga mnada ng’ombe 10,000 kutoka nchi za Uganda na Rwanda waliokamatwa katika operesheni inayoendelea nchini ya kukamata mifugo yote iliyoingizwa bila kufuata utaratibu.
Hayo yamesemwa hii leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wakati akichangia mpango wa Taifa wa maendeleo wa mwaka 2018/19, ambapo amesema kuwa ng’ombe hao watapigwa mnada wakati wowote, kama ilivyofanyika kwa ng’ombe 1,325 kutoka Kenya.
Amesema kuwa ushirikiano wa Tanzania na nchi zingine washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni mzuri na akasisitiza kuwa katika nchi hizo hakuna ushirikiano wa kihalifu bali upo wa maendeleo tu.
-
Askari waliobaka watoto wa miezi 18 wakalia kaa la moto
-
Bodi ya mikopo yatoa orodha mpya, wanufaika mkopo elimu ya juu
-
Bodi ya mikopo yatoa orodha mpya, wanufaika mkopo elimu ya juu
Hata hivyo, Mpina amesema kuwa walioingiza ng’ombe hao ni wahalifu na wamevunja sheria za nchi na kuwatahadharisha wafugaji wa nchi jirani kufuata sheria za nchi pindi wanapotaka kuingiza mifugo yao nchini.