Mbunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga amesema Serikali inapambana kutafuta wawekezaji kutoka nje na kuwainua wa ndani Kwa lengo la kutanua wigo wa ajira na kukuza uchumi wa Taifa.

Mahawanga ameyesema hayo Jijini Dar es Salam katika uzinduzi wa kampuni ya Kitanzania ya Asantemotors ambayo imetoa ajira Kwa watu zaidi ya 15.

Mbunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga.

Amesema, Wakulima wanatakiwa kujitokeza ili waweze kuagiza matreka kwaajili ya kilimo cha Biashara na kuachana na Kilimo cha mkono.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Asantemotors ametoa wito Kwa Serikali kuwashika mkono Wawekezaji wazawa, ili kuweza kuwainua na kukuza uchumi wa Taifa.

Taarifa utekelezaji REA III mzunguko wa pili yapokelewa
FAO yaunga mkono juhudi uendelezaji sekta ya Kilimo