Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amesema Serikali nchini, imetenga nafasi 30,000 za ajira kwa kada mbalimbali katika mwaka wa 2022/23.
Ndejembi ametoa kauli hiyo hii leo Novemba 10, 2022 Bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa mchakato wa kufanikisha ajira hizo unaendelea kama ulivyokusudiwa.
Kauli ya Ndejembi imekuja wakati akijibu swali la Mbunge Viti Maalum (CCM), Asia Halamga ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itaajiri wataalamu wa mazingira.
Akijibu swali hilo, Ndejembi alisema Serikali inakamilisha mchakato wa kuajiri watu 223 wa kada ya mazingira kwenye taasisi mbalimbali kwamba kwasasa wanaendelea kukamilisha taratibu husika.