Serikali ya Guinea ya Ikweta imetangaza kujiuzulu wakati mgogoro wa kiuchumi unaoendelea ambapo Rais Teodoro Obiang Nguema wa nchi hiyo amesikitwa na serikali hiyo kuwa inaondoka bila kufanikisha malengo yake iliyojipangia.
Rais huyo ambaye ameitawala nchi hiyo ndogo ya Afrika yenye utajiri wa mafuta kwa mkono wa chuma kwa takribani miongo minne, imeathirika pakubwa na mgogoro wa kiuchumi uliochochewa na janga la corona.
Serikali ilimkabidhi rais barua ya kujiuzulu wakati wa mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri.
Hata hivyo waziri mkuu Pascual Obama Asue, amesema imani ya kiongozi wa taifa inastahili watu kujitolea.