Muungano wa Walimu nchini Zimbabwe umekataa nyongeza ya mshahara ya asilimia 100 ukisema mshahara wa Dola 180 ni mdogo ikilinganishwa na kiwango cha umasikini ambacho kimefikia Dola 540
Serikali imetoa nyongeza hiyo katika jitihada za kuwataka warudi kazini baada ya wanafunzi kuwa wakienda shule kila siku, bila ya kuwepo masomo yanayoendelea kufuatia mgomo wa walimu.
Waziri wa Elimu, Amon Murwira amesema nyongeza hiyo ndio uwezo wa Serikali kwa sasa, akitumaini Walimu watakubali na kurejea Shuleni.
Mbali na ongezeko la mishahara, walimu wanataka vifaa vya kujikinga dhidi ya virusi vya Corona ili warejee Shuleni.