Mwenyekiti Serikali za Mitaa – Yombo Kiwalani, Muslim Dada ameishukuru Taasisi ya Datavision International kwa kuwafadhili na kuwasaidia kupata mkopo nafuu na rahisi kutoka Kampuni ya Kopafasta uliofanikisha ulipaji wa posho za walinzi wa mitaa.

Dodo ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao na kuongeza kuwa, Kopafasta kupitia Datavision wamewasaidia pia kuinua nguvu kazi na kuwaondolea adha ya ulipaji wa mikopo kwa Walinzi hao ambayo ilikuwa inasuasua na hivyo kudidimiza ari ya utendaji kazi.

Amesema, “ilikuwa ni kazi sana sisi kupata mkopo kutoka Kopafasta lakini kwa udhamini wa Datavision tukapata na niwashukuru sana viongozi wa matawi hapa Yombo pamoja na Vijana wa CCM kuunga mkono wa suala hili la ada shirikishi za ulinzi ambalo limeleta matokeo mazuri.”

Mwenyekiti Serikali za Mitaa – Yombo Kiwalani, Muslim Dada

Amesema, kupitia ada lipa kwa kipindi cha miaka mitatu (2021-2023), walifanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi 33 Milioni ambazo pia zimesaidia kuwalipa walinzi 32 kupitia mfumo huo wa ada lipa kwa michango ya shilingi 1,000 kwa kila kaya kulingana na eneo.

Hizi pesa zote hazitoki kwa Wananchi zinachangiwa na mfumo huo wa adalipa unaoratibiwa na Kopafasta ambazo zinakuwa salama na zinalipa kwa wakati hivyo kusaidia usalama na uhakika wa utendaji kazi usio na mashaka, tunawaomba tuendelee kujitoa ili tufike mbali zaidi,” amesema Dodo.

Awali, Mkurugenzi wa Miradi Datavision, Macmillan George alisema kampuni ya Datavision ndiyo inayoongoza kwa kufanya tafiti zenye matokeo chanya Tanzania, licha ya kwamba imekuwa ikisaidia kutafuta suluhu ya mambo mbalimbali yanayoikabili jamii hasa zenye uhitaji kulingana na mazingira na mifumo ya kieletroniki.

Mkurugenzi wa Miradi Datavision, Macmillan George.

“Na moja ya Tafiti ambazo tumekuwa tunajivunia sisi Datavision ilikuwa ni mwaka 2013 kama mtakumbuka tuliingia katika taharuki ya wanafunzi wengi wa shule ya msingi kwenda Sekondari ambao walikuwa hawajui kusoma na kuandika na uliifedhehesha taasisi nyingi sasa matokeo yake yalisaidia sana kuondoa tatizo hili,” amesema.

Aidha, ameongeza kuwa ulipiaji wa ada kwa njia ya simu ni salama na inasaidia kufanikisha malengo ambapo mta wa Yombo umechaguliwa kuwa mtaa wa mfano uliojiunga na mfumo wa ada lipa ukitumia gharama ndogo kwa uchangiaji wa kila kaya wenye matokeo mazuri ya ulipaji mishahara walinzi wa mtaa sawa na wanavyolipwa walinzi wa makampuni binafsi.

Ufadhili wa miradi GGML unavyoleta mageuzi kiuchumi Geita
Nasreddine Nabi: Bado tuna kazi kubwa Dar