Serikali imesema kuwa haioni sababu ya kuendelea kulumbana na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu.

Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas, kuhusu tuhuma zinazotolewa na Mbunge huyo kuhusu tukio la kushambuliwa kwake lililomsababishia majeraha makubwa.

Dkt. Abbas kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema kuwa Mbunge huyo bado ni mgonjwa na kwamba Serikali inaendelea kumuombea ili apone haraka aendelee na majukumu yake ya kila siku.

“Mhe Lissu bado ni mgonjwa na yuko wodini hivyo Serikali haioni busara kulumbana naye kwa sasa. Tunaendelea kumuombea apone haraka,”ameandika Dkt. Abbas katika ukurasa wake wa Twitter

Hata hivyo, Lissu ameendelea kutoa malalamiko yake na kusema kuwa kitendo cha yeye kupigwa risasi kuwa ni mipango iliyokuwa inalenga kumzimisha kabisaa ili asiendelee kuwasumbua.

 

Wafanyabiashara Mwanza wagoma
Magazeti ya Tanzania leo Januari 6, 2018