Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wajikite kwenye zao la kahawa ili wawe na zao mbadala la biashara.

 Ameyasema hayo hii leo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Lipokela na vijiji jirani, wilayani Songea mara baada ya kukagua shamba la kahawa la Aviv Tanzania lenye ukubwa wa hekta 1,990.

 “Limeni kahawa ili mpate fedha sababu zao hili ni la biashara. Kahawa ni miongoni mwa mazao matano ya biashara ambayo Serikali ya awamu ya tano imeamua kuyawekea mkazo ili yaweze kuongeza tija kwa wakulima na kuinua uchumi wa Taifa,”amesema Majaliwa

 Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa ni lazima wananchi walime zao hilo na viongozi wahakikishe wananchi wananufaika za zao hilo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Hata hivyo, ameonyesha kutoridhishwa na utendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea baada ya kuelezwa kuwa kampuni ya Aviv Tanzania imezalisha miche milioni moja lakini iliyochukuliwa na kusambazwa kwa wananchi ni miche isiyozidi 200,000.

 

Maandamano makubwa yafanyika Iran
Australia yapania kuwa muuzaji namba moja wa bangi duniani