Jaji Gerard Niyungeko, ambaye ameendesha kesi ya wanamuziki wa dansi nchini Papii Kocha na Babu Seya amesema mahakama imetoa mwezi mmoja kwa wanamuziki hao kuwasilisha madai ya fidia ikiwa watahitaji kulipwa gharama za kesi yao iliyokuwa inawakabili baada ya kuendeshwa bila kufuata misingi ya haki kikatiba.
Maamuzi hayo yamefanyika katika Mahakama ya Afrika ya Haki ya Binadamu, (AFCHPR), yaliyopo jijini Arusha.
Ambapo imeamriwa kuwa endapo wasanii hao watakubali kulipwa fidia ya gharama ya kesi hiyo, imetoa muda wa mwezi mmoja kwa Serikali kuwa tayari iwe imekwisha toa maamuzi juu ya madai hayo ya fidia.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya Mahakama ya Haki za Binadamu kubainisha kuwa mwenendo mzima wa kesi ya Babu Seya na mwanaye iliyoendeshwa katika Mahakama ya Tanzania na kusamimiwa na jopo la mawakili haikuzingatia vigezo.
-
Mahakama ya Tanzania yalaumiwa kutotenda haki kesi ya Babu Seya na mwanae
-
Serikali yakanusha kufungia mitandao ya kijamii
-
Video: Sura mpya kesi ya Babu Seya na mwanae, Watu wasiojulikana wavamia magereza
Baada ya walalamikaji kukosa haki yao ya kikatiba ya kuwa na familia zao na kuendelea na shughuli zao pia kesi yao imeonekana kukosa ushahidi wa athari hizo kutokana na maelezo yaliyofikishwa mahakamani.
Kesi hiyo ilisimamiwa na mawakili, Sara Mwaipopo, Nkosari Sarakikya, Baraka Luguna, Elisha Suka na Aida Kisumo.
Upande wa walalamikaji, mawakili waliowawasilisha ni Donald Deya ambaye ni mwanasheria na afisa mtendaji mkuu wa Chama cha Wanasheria wa Afrika.
Babu Seya na wanae watatu, walikamatwa Oktoba 12, 2003 na kufukishwa kituo cha polisi kwa tuhuma za ubakaji na ulawiti wa watoto wa kike wenye umri chini ya miaka 10, mnamo Juni 25, 2004 Mahakama ya Kisutu iliwahukumu adhabu ya kifungo cha maisha jela.
Babu Seya na wanae wametumukia kifungo cha jela kwa miaka 13, mpaka pale ulipotolewa msamaha wa rais, mnamo Disemba 9, 2017 katika sikukuu ya maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru wa Tanganyika yaliyofanyikia jijini Dodoma.