Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali haina mpango wowote wa kusitisha mbio za Mwenge wa Uhuru na kusisitiza kuwa dhana hii ni endelevu na itaendelea kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa kusisitiza misingi bila kuchoka.
Ameyasema hayo mapema hii leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge.
Amesema kuwa Kimataifa Mwenge wa Uhuru unaendelea kusimamia dhana na maudhui yake ya kumulika hata nje ya mipaka yetu kwa kuwa msuluhishi wa Amani Afrika na mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine Afrika na Dunia kote.
“Kutokana na faida na Mafanikio makubwa yanayopatikana kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru Serikali inaamini kuwa zipo faida nyingi ndani yake na mwenge huu utaendelea kudumu”,Amesema Mhagama.
Aidha amesisitiza kuwa Umoja, Mshikamano,Upendo na Ukarimu wa Watanzania ni alama tosha ya muungano wa Tanzania.
Hata hivyo, ameongeza kuwa Mwenge wa Uhuru unahamasisha na kuimarisha umuhimu wa Muungano kwa Watanzania wa pande mbili za nchi na kila mwaka huweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi na kuhamasisha uzalendo wa kuendelea kujitolea