Aliyekua mshambuliaji wa klabu Blackburn Rovers Chris Sutton, amesema kitendo cha Meneja wa Manchester United Jose Mourinho kuhoji uwajibikaji wa wachezaji wake ni dharau na kuwashusha thamani nyota hao.

Mourinho amekosoa hadharani kitendo cha mabeki Luke Shaw, Chris Smalling na Phil Jones kurudi katika majeruhi mara kwa mara.

Sutton ameiambia BBC Radio 5 live kuwa Mourinho angekuwa anakutana na hatari dhidi yake kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kama angekuwa mchezaji wake.

“Kuwaambia wachezaji kuwa hawapendi kucheza wakati wameumia sio sawa kabisa. Makocha niliowahi kucheza chini yao wanazungumza ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo lakini Mourinho anasema hadharani. Nadhani anasababisha matatizo.”

“Anaiambia bodi ya klabu kuwa wachezaji hawa siwataki nahitaji mbadala wao. Hafikirii anachotaka kusema. Mourinho katika siku za karibuni ametoa kauli za kuwakosoa wachezaji wake hadharani,” Alisema Sutton.

Akizungumza kuhusu Shaw mwezi uliopita Mourinho alisema: “Siwezi kumlinganisha jinsi anavyofanya mazoezi, anavyofikiri na kujituma. Yuko nyuma sana.”

Hii ilikuwa baada ya sare dhidi ya Swansea City kwenye mkutano wa waandishi wa habari ambapo pia alisema: “Sipendi kuzungumza kuhusu Phil Jones na Chris Smalling. Napenda kuzungumza kuhusu Juan Mata ambaye atanipa kila kitu akiwa uwanjani. Nina shukuru kwa hilo.”

Wakandarasi wa ndani kunufaika na miradi isiyozidi thamani ya bilioni 10
Serikali yapigilia msumari wa moto kuhusu mwenge