Mkutano wa mashauriano wa Bodi ya usajili wa makandarasi wa mwaka 2017 umefunguliwa mapema hii leo mjini Dodoma na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na kuagiza kuwa miradi yote yenye thamani isiyozidi bilioni 10 wapewe Wakandarasi wa ndani.

Amesema kuwa wakandarasi hao wapewe miradi hiyo ili waweze kudharisha ajira kwa vijana wengi wa kitanzania waliopo mtaani.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa ili wathubutu kujitosa na kumudu zabuni za ujenzi kwani kwa kufanya hivyo kutaleta faida mbalimbali ikiwemo fedha watakazopata kwani wataweza kuwekeza ndani ya nchi na kutoa ajira.

“Hatuwezi kuwa na Tanzania ya Viwanda huku tukiwanufaisha Makandarasi wa nje pekee ni lazima Makandarasi wa ndani wanufaike pia.”amesema Samia Suluhu.

Aidha, Makamu wa Rais ameahidi kuwa Serikali itaendelea kulipa madeni inayodaiwa na wakandarasi ili kujenga mahusiano mazuri ya wakandarasi hao.

Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa kuwa Wizara hiyo inaendelea kusimamia sheria na maadili kwa wakandarasi ili kuhakikisha miradi ya ujenzi inayotekelezwa kote inakuwa na ubora unaotakiwa.

 

Kwa upande wake, Msajili wa Bodi ya Wakandarasi Nchini, Rhoben Nkori amesema bodi hiyo imefuta usajili wa wakandarasi 3,000 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Usajili wa Wakandarasi ya mwaka 1997 na kwa sasa bodi hiyo inawakandarasi 9,000 kote nchini.

 

Video: Hussein Machozi Aachia Video ya ‘Nipe Sikuachi’
Chris Sutton: Jose Mourinho Aheshimu Wachezaji