Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameongeza wiki mbili nyingine za “lockdown” kama njia mojawapo ya kupunguza maambukizi ya Covid- 19 katika nchi hiyo .
Rais Ramaphosa amesema kuwa shule zitaendelea kufungwa na kuendelea kuzuia mikusanyiko katika sehemu mbalimbali ikiwemo sehemu za starehe, hatua hiyo imekuja kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini Afrika ya Kusini.
Aidha sehemu za mazoezi na migahawa katika sehemu mbalimbali ya miji nchini humo ikiruhusiwa kufunguliwa kwa sharti la wateja wao kukaa mbalimbali.
“Serikali itaongeza fedha katika mfuko wa Covid ili kufidia biashara zilizoathiriwa,” amesema Rais Ramaphosa.
Mpaka hivi sasa Afrika Kusini imeripoti maambukizi mapya 16,302 ambapo siku ya Jumapili jumla ya idadi ya maambukizi imefikia 2,195,599.
Jana watu 151 walifariki kwa sababu ya Covid na kusababisha idadi ya vifo kufikia 64,289