Serikali kupitia Wizara ya Afya imewata Mawaziri wa Afya Afrika kutambua kuwa Sekta ya afya ina mahitaji mengi na muhimu kwa nchi zinazoendelea hivyo hawana budi kuwekeza kwenye vipaumbele vichache hasa vinavyohusu kuimarisha huduma za Afya ya Mama na Mtoto
Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Ummy Mwalimu katika Mkutano wa 4 wa Kuondoa vikwazo katika kuokoa Maisha ya Mama na Mtoto.
Amesema kuwa mipango mbalimbali na changamoto ambazo Tanzania na nchi nyingi za Kiafrika zinakabiliwa nazo katika kufikia mipango endelevu ya upatikanaji wa rasimali fedha katika kutekeleza afua mbambali za sekta ya Afya.
“Katika mkutano huu ambao umefunguliwa na Dkt. Mulatu Teshome, Rais wa Jamhuri ya watu wa Ethiopia unajadili masuala mbalimbali ikiwemo mikakati ya kumaliza vifo vya mama na mtoto, kuongeza usawa katika upatikanaji wa huduma za Afya kwa kuondoa vikwazo, kuboresha ubora wa huduma za afya na kuimarisha matumizi ya takwimu katika kupanga mipango ya utoaji wa huduma za Afya,”amesema Ummy
-
Madaktari mbaroni kwa biashara ya viungo vya binadamu
-
Aliyefungwa jela Miaka 25 kwa mauaji ya kusingiziwa adai mabilioni
-
RC Makalla awapiga kitanzi wakurugenzi Mbeya
Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania imeanzisha mikakati mbalimbali ya kuhakikisha fedha kidogo zilizopo zinatumika vizuri ikiwemo kutoa fedha kwa Vituo vya huduma kulingana na matokeo/utendaji wao (Result Based Financing) ambapo vituo vya tiba vilivyokuwa na hali mbaya (nyota sifuri) vinapewa fedha kuboresha huduma ambapo maboresho makubwa yameonekana katika vituo hivyo ndani ya kipindi kifupi.