Afisa Biashara wa mkoa wa Dar es Salaam, Thabit Massa, amewataka wafanyabiashara wa mbolea kuhakikisha mbolea wanazowauzia wakulima zina viwango sahihi visivyoweza kusababisha athari kwenye mazao.
Thabit ametoa wito huo leo Septemba 21, 2020 Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na wafanyabiashara wa mbolea kutoka Temeke na Kigamboni katika mkutano ambao utawasaidia wafanyabiashara hao kuelewa malengo ya serikali katika kipindi hiki cha uchumi wa viwanda.
Kwa upande wao wafanyabiashara hao wa mbolea wameeleza changamoto wanazokutana nazo wanapofika kwa wakulima kuwauzia mbolea kuwa ni pamoja na wakulima kutaka mbolea ya kilo moja moja ama tano wakati wao wana mbolea iliyofungashwa kwenye mifuko ya kilo 50.
“Tunahitaji wafanyabiashara wazalishe mbolea zenye viwango ili kukidhi soko la kimataifa”, Amesema Thabit.