Kiwanda cha kuchakata takataka kinatarajiwa kujengwa  jijini Dar es salaam kwa msaada wa Ujerumani ambapo takataka hizo zitakuwa zinabadilishwa kuwa mbolea ambayo itagawiwa kwa wakulima.

Hayo yamesemwa na Meya wa Kinondoni, Benjamin Sitta alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kiwanda hicho kitazalisha ajira kwa wingi kwani kitahitaji wataalamu kwa wingi.

“Mradi huu wa kujenga kiwanda kitakuwa na faida kubwa, si tu kwa wananchi wa Kinondoni bali utasaidia kwa jiji zima la Dar es salaam kwani tutakuwa tumeondoa kero kubwa ya takataka majumbani,”amesema Sitta

Hata hivyo, Sitta ameongeza kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utasaidia kuzalisha ajira kwa wingi na kuokoa uchafuzi wa mazingira katika jiji la Dar es salaam ambalo ndilo kivutio kikubwa kwa Tanzania.

 

 

Simba yaomba radhi mashabiki wake
Video: RC Makonda kuwakwamua Waalimu, aahidi kufanya makubwa