Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wanaotuhumiwa kwa makosa ya ugaidi, ambapo leo Novemba 2, 2021 inaendelea kuunguruma katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Mahakama hiyo inatarajiwa kuendelea kupokea ushahidi wa upande wa mashtaka kutoka kwa shahidi wa tano.
Tayari washtakiwa wameshafikishwa mahakamani na wako mahabusu wakisubiri muda wa kupandishwa kizimbani.
Endelea kufuatilia Dar24 Media, Tutaendelea kukuletea mwenendo wa kesi hii.