Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado shaibu amesema Wanasiasa nchini wameufurahia uelekeo mpya wa kisiasa ambao umeletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuondoa zuio haramu la kufanyika kwa mikutano ya hadhara
Shaibu amesema hayo katika mahojiano maalum na Dar24 Media, ambapo amesema shughuli za kisiasa nchini zinaendeshwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Sheria ya Vyama vya Siasa pamoja na kanuni zake.
Amesema, ”Katiba sheria ya vyama vya siasa vyote hivi ukivisoma kwa pamoja utaona kwamba vinaruhusu vyama vya siasa vyote nchi kufanya shughuli zake ikiwemo mikutano ya hadhara maandamano, makongamano pamoja na vikao vya ndani.”
Ameongeza kuwa, ”Uwamuzi wa serikali ya awamu ya tano mwaka 2016 kuzia kufanyika kwa mikutano ya hadhara kwa kisingizio cha kwamba mikutano ifanyike wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzina wakati wa shughuli za maendeleo vilikuwa havina msingi wa kisheria wala kikatiba.”
”Tulikuwa na matumaini ya muelekeo mzuri wa kisiasa kwa mwaka 2023 lakini hatukuwa na uhakika kwamba maamuzi haya mazuri yatakuja mwezi Januari na Rais ametu ‘suprise’ kwa chama chochote makini baada ya zuio lile kuondolewa tunapaswa kurudi kwenye vikao vya chama na kuhakikisha kunakuwa na mikutano yenye tija,” amebainisha Shaibu.
Kuhusu mikakati ya ACT Wazalendo, mara baada ya zuio la mikutano ya hadhara kuondolewa Shaibu amesema, “Kama chama tunajipanga kwenye vikao vyetu na tunaamini kwamba mapaka kufikia katikati ya mwezi wa kwanza mtakuwa mshapata muelekeo na watu wajiandae kuona kishindo cha Act Wazlendo.”