Vyombo vya Usalama nchini Ukraine, vimesema watu sita wameuwawa katika shambulizi la kombora kutoka upande wa Urusi, lililolenga jengo la makazi kwenye mji wa kusini wa Mykolaiv.

Meya wa Mykolaiv, Oleksandr Senkevych amesema vikosi vya uokozi vinaendelea na juhudi za kuwatafuta manusura wa shambulizi hilo, ambapo rais Volodymyr Zelensky amelitaja kuwa jibu la kikatili kutoka kwa Urusi kutokana na mafanikio ya vikosi vya Ukraine kwenye uwanja wa vita.

Mwananchi mmoja akisaidia kuzima moto katika mji wa Bakhmut kufuatia shambulio la anga. Picha ya Igor TKACHEV / AFP.

Aidha, shambulizi hilo limetokea wakati Urusi ikiwa tayari imetangaza kuwa inaondoa wanajeshi wake kutoka mji wa Kherson, ambao Moscow iliukamata katika siku za mwanzo za uvamizi wake nchini Ukraine mapema mwezi Februari.

Hata hivyo, Ukraine imedai kwamba vikosi vyake vinasonga mbele kwenye maeneo kadhaa ya mapambano, licha ya hujuma za vikosi vya kijeshi toka nchini Urusi.

NECTA yatakiwa kuimarisha usimamizi changamoto za mitihani
Majaliwa atinga Bungeni, Spika ampongeza