Mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, na kundi la waasi wa M23 Wilayani Rutshuru, yamechochea hamasa ya vijana wengi wa mkoa wa Kivu Kaskazini kujiandikisha jeshini.

Hamasa hiyo, imejiri wakati jeshi la Kongo likiendelea na mashambulizi ya anga yanayolenga maeneo yanayodhibitiwa na waasi, hali ambayo inayowalazimu raia wengi kuelekea mjini Goma kukimbia mapigano.

Vijana wenye hamasa waliojitokeza kujiunga na Jeshi la DRC kupambana na waasi wa M23. Picha ya Michael Lunanga / AFP.

Baadhi ya vijana hao, wengi wakitoka maeneo yanayokumbwa na vita, wanasema hiyo ni njia ya kuliongezea nguvu jeshi la congo ili kupambana na kundi la waasi wa M23 wanao daiwa kupata usaidizi kutoka nchi jirani ya Rwanda, madai ambayo Rwanda imeyakanusha.

Hata hivyo, Vijana kutoka wilaya ya Beni, butembo ,rutshuru na maeneo mengine ya mkoani kivu kaskazini wanao kadiriwa kuwa zaidi ya 3,000, wanasema wana lengo la kuyatokomeza makundi yote ya waasi yanayo yumbisha usalama wa wananchi wa eneo la Mashariki mwa Congo.

Mtaturu aibana Serikali ujenzi Kituo cha Polisi
Majaliwa ataka tafiti zaidi kubaini vyanzo vya maji