Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ameihoji serikali kuhusu kiasi cha fedha kilichotengwa Shilingi Bilioni 1.1 kwa ajili ya kujenga kituo cha polisi cha Ikungi, ni lini kitapelekwa ili kuanza kwa ujenzi wake.

Mtaturu ametoa kauli hiyo hii leo Novemba 10, 2022 Bungeni jijini Dodoma, na kusema “Tulipitisha hapa bungeni bajeti ya Shilingi Bilioni 1.1 kwa ajili ya kujenga kituo cha Polisi Ikungi, leo ni mwezi wa 11 je ni lini serikali italeta fedha kwa ajili ya kujenga kituo hicho.”

Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amekiri kupitishwa kwa bajeti hiyo ajili ya ujenzi wa kituo hicho na kudai kuwa, “Jeshi la Polisi limewasilisha mpango kazi wa ujenzi ambao utakapopitishwa na wizara utawasilishwa hazina kwa ajili ya kuidhinisha fedha.”

Ameongeza kuwa, “Ni imani yetu fedha za maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki kwa vile zinatoka kwenye mfuko ambao tuliuzungumzia kikamilifu wiki iliyopita, zitatoka kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa kituo hicho kuanza.”

Serikali kuchimba visima kukabili uhaba wa Maji
Mapigano yachochea Vijana kujiunga na Jeshi