Tukio la shambulizi, linalohisiwa kufanywa na wenye itikadi kali huko magharbi mwa nchi ya Burkina Faso limesababisha vifo vya watu 33.
Gavana wa jimbo la Mouhoun nchini humo, Babo Pierre Bassinga amesema jitihada za kiusalama dhidi ya watu wenye itikadi kali ulitokea katika kijiji cha Youlou zinaendelea.
Aidha, amesema mbali na juhudi hizo anawataka wananchi kuchukua tahadhari na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama.
Matukio kadhaa yaliyoleta madhara au kusababisha taharuki, yamekuwa yakihusishwa moja kwa moja na watu wenye itikadi kali ambao wanapingana na sheria za Serikali.